FLAVIANA MATATA FOUNDATION YAZINDULIWA USIKU HUU...!!!

 Mwanamitindo Flaviana Matata anayefanya kazi zake nchini Marekani akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa taasisi yake inayoitwa Flaviana Matata Foundation, ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kusaidia na kusomesha watoto wa kike wasiojiweza na wasiokuwa na wazazi au walezi, Flaviana amesema taasisi hiyo itafanya kazi kwa karibu na watu mbalimbali hapa nchini ambao wamekuwa wakisaidia jamii yenye matatizo mbalimbali. Uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali maarufu nchini wakiwemo wabunge na viongozi wa serikali umefanyika usiku huu kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na wageni waalikwa katika uzinduzi huo usiku huu.
 Mkurugenzi wa Utamaduni katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko akizungumza na wageni waalikwa.
 Mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Marekani Hasheem Thabit katikati akiwa katika picha ya pamoja na mbunifu Ali Remtullah kulia na Jokate Mwegelo katika uzinduzi huo.
 Mbunge wa Singida Mjini CCM Mohammed Dewji akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mwasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda
Kutoka kulia ni Khadija Mwanamboka wa TMH, kushoto ni Fiderine Iranga na Christine Mosha Seven wa MTV Base na mdau ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga Mh. Januari Makamba akiteta jambo na mwendeshaji wa mtandao wa www.hakingowi.blogspot.com Bw. Haki Ngowi. 
 Kutoka kulia ni mmiliki wa Taasisi ya (Flaviana Matata Foundation) Flaviana Matata Ruge Mutahaba Mkurugenzi wa Radio Clouds na Mbunge wa jimbo la Bumbuli CCM Mhe. Januari Makamba.
 Mkurugenzi wa Masoko na mwasiliano wa. Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa katika picha ya pamoja na mwanamitindo Flaviana Matata ambaye amezindua rasmi taasisi yake ya kusaidia watoto wakike wenye matatizo hasa katika suala zima la kuwasomesha
 Mwendeshaji wa mtandao wa Bongocerebrity Jeff Msangi akiwa katika picha ya pamoja na mwandaaji wa mashindano ya Miss Universe Maria Sarungi.
 Hawa wadau nao walikuwepo katika uzinduzi kutoka kulia ni Mohamed Jamalee wa Farm Plant, mdau Gonzaga, na Mdau Ben Mulokozi.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Serengeti SBL Teddy Mapunda akipozi katika picha na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Radio Clouds Barbara Hassan. 
 Kutoka kushoto ni Mr Ido, Mwamvua Mlangwa wa Vodacom Tanzania, Maria Sarungi, Joseline Kamuhanda wa Vodacom Tanzania na Lilian wa Vodacom Tanzania pia wakifuatilia matukiao mbalimbali katika uzinduzi huo.
 Kutoka ushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti (SBL) Teddy Mapunda, Barbara Hassan wa Clouds na Salam Jabir wakifurahia jambo.
 Wadau wa Miss Tanzania nao walimpiga tafu Flaviana Matata kutoka kulia ni Bosco Majaliwa katibu Mkuu Miss Tanzania, Kissa aliyewahi kushiriki katika mashindano ya Miss Tanzania na owner of KIKI'S, Hashim Lundenga mkurugenzi Miss Tanzania na Mdau Selemani Mbuguni wa Gazeti la Majira.
Flaviana Matata akipiga picha na viongozi mbalimbali ambao watamsaidia katika majukumu yake kuhusu taasisi hiyo.

Image credit: Full Shangwe

Comments