IRENE UWOYA ADAI BADO ANADATISHAAAA...!!!

Msanii ‘high class’ wa filamu Bongo, Irene Uwoya ‘Mama Krish’ ameibuka na kueleza kuwa, licha ya kujifungua hajakongoroka kama inavyokuwa kwa wanawake wengine.
Uwoya alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na gazeti hili na kudai kuwa, kinachomsaidia kuwa hivyo ni kufanya mazoezi kila anapopata nafasi.


“Nimejifungua na ninanyonyesha lakini sijapoteza mwonekano wangu, bado nina mvuto kama unavyoniona. “Kwa hiyo ile dhana kwamba mwanamke akijifungua anakongoroka kwangu haina nafasi, sibweteki, nafanya mazoezi na nakula vizuri ndiyo maana niko hivi,” alisema…

Source: GPL

Comments