Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Pembeni ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga aliyemkaribisha Mhe. Spika Ubalozini.
pika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiangalia picha mbalimbali za Mabalozi wa Tanzania waliowahi kuhudumia Ubalozi wetu tangu Uhuru nchini Uingereza zilivyopambwa katika ngazi za kuingia Ubalozini hapo mara baada ya kutembelea Ubalozi huo Leo. Anaemuongoza kuingia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga mara baada ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Pembeni ni mjumbe wa kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Beatrice Shelukindo aliyekuwa ameambatana na Mhe. Spika.
Spika wa bunge Mhe Anne Makinda akiwa katika mazungumzo na maafisa wa ubalozi wa Tanzania Nchini Uingereza wakati alipotembelea ubalozi huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga pamoja na watumishi wote wa Ubalozi wetu nchini Uingereza mara baada ya kutembelea Ubalozi wetu Uingereza.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
Comments
Post a Comment