ALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye
pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti na mkoa wa Ilala kimichezo
amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wa
ngumi katika kipindi cha mwaka 2011.
Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha
wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la
Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi
na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.
Alisema pamoja na hilo pia ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi
pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa
mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali
yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.
Katika hatua nyingine Super D amekua akitoa mafunzo ya mchezo wa
ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali kwa njia ya DVD
zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala 'Super
D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na
mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri
Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo
kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa
ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya
utangulizi.
Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua
mabondia wengine chipkizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu
Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa
vipaji vyao.
Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga Mustapha Doto,kwa pointi
60-57 alishinda ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya
utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward
lililofanyika DEsemba 25 mwaka huu.

Comments
Post a Comment