ISSUE YA MATUMIZI YA MAJINA YA MASTAR WA NJE NA MASTAR HASA WA KIKE NYUMBANI TZ...!!!

Wapenzi wasomaji wangu leo nakuja kivingine naomba tuongelee hili suala la watu hasa ma celebrity wetu huko Tanzania kujiita au kutumia majina ya mastar wengine wa ulaya! Je hii ni sawa?

Mimi binafsi naona si sawa na sioni sababu ya mtu kujiita sijui Beyonce, J Lo, Lady Gaga, Kim K, Nicki Minaj nk. wakati mtu ana jina lake na ni zuri tu na pia anweza kulikuza kama hawa mastar ambao ndo idols zao as they say au wanao jifananisha nao.

Najua kuna wengine wamepewa na marafiki zao hayo majina ila kwa nini mtu asiwe proud na jina lake? Unakuta mtu kakazana kazana tena haswa kulikuza na kujiita hilo jina la huyo star wa nje wakati mwenzake jina tayari analo!

Na kaitika pita pita zangu facebook nilikutana na mdau aka tena bongo celebrity mwingine ambaye nae alikuwa ana mawazo kama yangu na yeye aliandika hivi: 
"Jamani wats this mastar wabongo kujiita majina ya macelebrity wa nje like keri hilson,minaj,tyra banks,kimora lee,jlo,rihhana,beyonce n whatsoever?to ♍ε its a big NO kwa  kweli au labda mie mshamba nisaidiwe lol"

Napenda kuwakilisha na pia naombeni maoni yenu wadau.

"BE PROUD OF YOUR NAME & ROCK IT"

JG 
xoxoxox

Comments

  1. Asante sana jestina kwa kuleta hili swala linakera sana unakuta mtu anajiita jina la mtu hata hawafanani wala mueleko hakuna haihusu kabisa.

    ReplyDelete
  2. Hakuna anayejiita a.k.a Mubelwa Bandio?
    Duh !
    Kwanza watu wajiulize KWANINI WANA MAJINA WALIYONAYO kisha wafikirie UMUHIMU wa kuyabadili.

    ReplyDelete
  3. yaani umenifurahisha sana sana, mimi ni bloger mwenzio (jina kapuni) lol, kwa kweli ni aibu aibu, na kwangu mie huu mtindo wa kujiita majina ya nje ni kulazimisha kujulikana. kwanini mtu usitumie jina lako?

    ni ulimbukeni kabisaaaaaa, halafu hawana hata aibu jamani lol..umenikosha leo. hongera kwa kazi nzuri sis......

    ReplyDelete
  4. yaani umenifurahisha sana sana, mimi ni bloger mwenzio (jina kapuni) lol, kwa kweli ni aibu aibu, na kwangu mie huu mtindo wa kujiita majina ya nje ni kulazimisha kujulikana. kwanini mtu usitumie jina lako?

    ni ulimbukeni kabisaaaaaa, halafu hawana hata aibu jamani lol..umenikosha leo. hongera kwa kazi nzuri sis......

    ReplyDelete
  5. Huko ni kutokujitambua, kujiona dhalili yani wanawaona macelebrity wa ulaya ni bora kuliko wao. na ndio maana mastaa wetu bongo hawaheshimiki, yani tunawachukulia poa tu.

    ReplyDelete
  6. Hiyo inatokana na mtu kutojielewa identity yake i.e. yeye ni nani hasa. Pia mtu anapojaribu kuwa kama fulani ndio hapo wanaanza kujiita majina ya watu. Mimi binafsi siamini kama mtu unaweza kuwa kama mtu fulani; lakinin unaweza kuwa the best you can be. Naamini Mungu amemuumba kila mtu na identity yake, na anaelewa destination zetu pia. You just have to work hard to archieve kile kilichokuwa destined kwako au kile unachopenda kuwa. Unaweza kuwa the best model lakini sio lazima uitwe Tyra au Naomi for that matter. Same applies to movie stars and the like. It is worth to make a name for yourself and not carry over someone's name. Lakini at the sametime tukumbuke; kila mtu ana-choice yake pia. Life is about choices and decisions we make. One's cup of tea may not be another person's cup of tea. At least this is how I see it!

    ReplyDelete
  7. Umefaanya vizuri sana dada kutoa hii mada, sielewi kwa nini mastaa wetu wa nyumbani wanapenda sana majina ya majuu, huu ni ushamba dada kabisa na wala haipendezi kabisa, kwa nini wasijiite majina yao asilia na wakawa proud kwa vizazi vipya pia, unajua hata ukiijiita JLo, Amber Rose, utabakia vile vile kama mbongo huwezi kuwa Jlo hata kidogo, hebu tudumisheni utamaduni wetu jamani kwa wale wenye tabia ya kubadili majina ya majuu.

    ReplyDelete
  8. yaani inakera ile mbaya sijui kwanini hawataki majina yao!!?mbona wakina wema sepetu na jokate wanatumia majina yao na yamekua makubwa tu!!!!?halaf hawa movie star wakibongo na hiyo mirangi ya ajabu ajabu kwenyenywele zao utasema wanaimba rock n roll hata hawapendezi!!!!!!!!!!!!kwanini hawajifunzi muonekano km wa halle berry 'nia long gabrielle union

    ReplyDelete
  9. Umesema ukweli! It seems like we are proud of ourselves. Tanzania tuna watu wazuri. We need to embrace ourselves tuanche kuiga sana.

    ReplyDelete
  10. Huwa ni Maattention seeker.

    ReplyDelete
  11. Yote ni kutojiamini wanajua majina Yao hayatawatoa

    ReplyDelete
  12. hawana cha ustaa wowote! n ushamba 100%

    ReplyDelete
  13. mii luv my name

    ReplyDelete
  14. Halfau kwa nini kama wantaka majina mengien waijitungie ya kwao wanaboa sana

    ReplyDelete
  15. Heeeee heee.Yaani me nikishasikia jina la bandia halafu nauna sura ya mtu hata siye...basi hata sitaki kusikia habari zake maana kwanza arejee aka-sort out jina lake kabla sijasikia habari zake.Cheee!Ni nini lakini jamani???How can they move fwd na fake names???Wanamkuza huyo celebrity wanaetumia jina lake badala ya kujikuza wao...upeo mdogo sana.Hivi wenzetu hawa wanajua BRAND?Inabidi wapate shule kdogo ya hii kitu.Hata kama hawataki kutumia majina yao,basi watengeneze Brand behind their names na waikuze.Tazama Diamond...jina lake nani tena?Me hata silijui...Ila nikisikia Diamond najua ni nani ana sura gani miziki yake.Na naona yeye kidogo kaelewa biashara na Brand,japo hajatumia jina lake halisi lakini katumia Diamond kama Brand behind his name.Hakurukia jina lamtu aliyekwisha jitengenezea jina katika fani yake.

    ReplyDelete
  16. hehehehheehehheh.. kazi kwelikweli na "so-called mastar bongo"yaani ni aibuuuuuu.. eti kim k inahusu.

    ReplyDelete
  17. tena wengine wanajipa majina wakati huko majuu watu hawataki hata kuyasikia kutokana na matendo machafu walonayo! kim k ana kashfa ngapi au yy mbongo yupo hivyo?? amber rose,jlo??? whaaat??? kwakweli ni kutojiamini kabisa,anyways may b someday watazinduka kutoka huo uzingizi mnono walolala!! wanabore kiasi ambacho hakielezeki!

    ReplyDelete
  18. kwa upande wangu mimi naona ni kutojiamini na kutolipenda jina lako halisi, pia ni kutengeneza tension,why wao hawajiiti ya kwetu? tutengeneze majina yetu, ndo mpango mzima

    ReplyDelete
  19. Hahahaa mi naonaga ni vituko tu.Mtu inakuwaje uwe comfortable kujiita jina la mwingine?Huko ni kutokujiamini,na pia ni kujikataa..Imagine mtu unajiita labda KIm Dash,alafu Kim anaoneshwa picha yako anaangua kilio,kwamba u don look like her.Hivi utajiskiaje?Anyway,ni uamuzi wao.tuwaache tu.

    ReplyDelete
  20. Its sad napia inaonesha mastar wa kike bongo hawana self-esteem mana huwezi kujiita jina la mtu mwingine ambae hufanani nae...sijui Kim K, Jlo sijui nani. Kwann usiwe comfortable mwenyewe na jina lako kwani hao wote wanajiirefusha herwfu zao tuu lkn hawana originality kma ustaa wao. Inabidi waache wanaboa.

    ReplyDelete
  21. Huo ni ushamba yaani usio na kifani. Kwanza unajiita jina na kujifananisha na watu marufu wa nje wakati hata hawafanani. Najua wote binadaam lakini kwa mambo mengine ni shame..eti Jlo, Kim K whaaat!!! Full ushamba...

    ReplyDelete
  22. Jestina mimi sikua na pa kusemea tu,bora umesema wewe....
    Ni washamba,wajinga na wagumu kuelewa
    Halafu wameambiwa hapa wanaliaje?
    Eti wanafatwafatwa...uuwiiii!
    Hebu mjifunze wabongo wenzangu

    ReplyDelete

Post a Comment