MUNGU ni mkubwa! Hatimaye dua za Watanzania zimesikika kwa staa wa Kundi la Orijino Komedi aliyepo Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu, Joseph Shamba ‘Vengu’ (pichani) ambaye ameinuka na kukaa mwenyewe kitandani, Amani limehakikishiwa.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambaye ni mtu wake wa karibu, mbali na hatua hiyo, pia nyota huyo ameanzishiwa mazoezi ya kuongea baada ya kitambo kirefu kutomudu kuzungumza.
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa, jitihada kubwa zilifanywa na madaktari wa Hospitali ya Appolo ili kuhakikisha kuwa Vengu anarudi katika hali yake ya kawaida.
Habari zaidi zilisema kuwa kinachomfanya Vengu kushindwa kuzungumza vizuri ni kupoteza kumbukumbu kwa muda mrefu na kufanya mdomo wake kuwa mzito.
Mbali na kufanyishwa zoezi hilo la kuzungumza, pia Vengu ameanza kufanyishwa mazoezi ya viungo ili kumfanya aweze kutembea mwenyewe.
“Madaktari wameonekana kufurahishwa na hatua hiyo na wanamfanyisha mazoezi ya viungo na kumzoesha kuongea kama unavyojua ana siku nyingi hajazungumza,” kilisema.
Hata hivyo, Amani lilifanikiwa kumpata mchumba wa Vengu ambaye ni Miss Kinondoni 2011/12, Stella Mbuge na kumuuliza kama ana taarifa zozote kuhusiana na mgonjwa huyo, naye alisema ameambiwa na kaka wa Vengu kuwa sasa jamaa yake yuko katika hatua ya kufanyishwa mazoezi ya kuongea.
“Kaka yake amefurahishwa na hali ya Vengu na amenihakikishia kwamba qnaendelea vizuri, kwa sasa anaweza kuinuka na kukaa mwenyewe ila wanamfanyia mazoezi aweze kuongea tena,” alisema kwa kifupi Stella.
Source: Global Publishers

Jaman hizi Habari kuhusu VENGU ni zakeli maana kwenye Mtandao wa FB zinasambaa Habari Mbaya kidogo
ReplyDelete