REDD'S MISS UNI-COLLEGE TEMEKE 2013

 Mazoezi ya mwisho  mwisho...
Warembo wa shindano la Redd's Miss Uni-College Temeke 2013 wakiwa kwenye picha tofauti mapema leo wakati wa mazoezi yao ya mwisho ndani ya ukumbi wa Kimataifa wa Club Bilicanas, Posta Jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia fainali hizo, Mratibu wa shindano hilo , Florence Josephat, alisema kuwa maandalizi ya shughuli hiyo yameshakamilika na tayari warembo wote zaidi ya 14,  wamejifua vya kutosha.
Florence alisema kuwa ni kinyang’anyiro hicho kitakuwa cha hali ya juu  na wadau wa burudani watapata wasaha  wa kushuhudia warembo hao sambamba na burudani kutoka kwa Ben Pol ambaye anatamba na vibo mbalimbali ikiwemo kibao chake kinachotamba kwa sasa cha ‘Jikubali’.
Aidha, Florence alitamba kuwa, kutokana na ubora wa warembo walionao, wana imani mwaka huu Redd’s Miss Tanzania atatoka katika kitongoji chao hivyo kuwataka  wadau kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti hasa wanafunzi mbalimbali wakiwemo wale wa vyuo ambapo kiingilio siku hiyo kitakuwa sh 10,000.
Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia ya TBL, kupitia kinywaji chake cha Redd’s  Orijino, Bilicanas, Tanzania Fame Company Ltd, Ndio Fashion, Robbyone fashion, Shome Decoration & Catering, djfetty.blogspot.com, Lamada Hotel na wengine wengi.

Comments