Inarepotiwa kwamba mama mmoja amepigwa risasi na polisi kujeruhiwa vibaya maeneo ya mapato Arusha.
Chanzo cha tukio hilo kinasema kwamba mama huyo alifika maeneo hayo na kupaki gari yake akitaka kuingia bank lakini akaambiwa eneo hilo halifai kupaki gari. Habari zinaendela kudai kawmba mama huyo alipaki gari na kuingia bank alipotoka alikuta gari lake limetolewa upepo na ndipo vurugu ilianzaa baina yake yeye na polisi.
Vurugu ilipokuwa kubwa mama huyo aliwaambia polisi kwamba wasimtishie bunduki hata yeye anayo na alipotaka kuitoa polisi wakampiga risasi.
Mama huyo ni muuzaji maarufu wa madini jijini Arusha na amekimbizwa hospitali na yupo chumba cha upasuaji.

Comments
Post a Comment