![]() |
| Baadhi ya miili ya watu waliokufa kwenye ajali iliyosababishwa na basi la Sumry |
![]() |
| Ndugu, jamaa na familia za marehemu wa ajali iliyosababishwa na basi la Sumry wakiwa nje ya hospitali kusubiri kutambua miili ya ndugu zao |
MIILI
ya watu waliofariki kwenye ajali iliyosababishwa na basi la Sumry,
iliyoaua watu 19 wakiwamo trafiki wanne imeanza kutambuliwa.
Ajali
hiyo ilitokea juzi kwa basi la Sumry lililokuwa linatokea Kigoma kwenda
Dar baada ya kuwaparamia watu waliokuwa wakitoa msaada ya mwendesha
baiskeli aliyekuwa amekufa kwa kugongwa katika kijiji cha kijiji cha
Utaho, wilayani Ikungi, barabara kuu ya Singida- Dodoma.
Kwa mujibu
wa Kamanda wa Polisi Mkoa Singida, Geofrey Kamwela, alisema siku ya
tukio hilo wananchi wakiwa na askari polisi wa doria walikuwa
wamekusanyika pembezoni mwa barabara kuupakia mwili wa mwendesha
baiskeli, Gerald Zefania, aliyegongwa na lori na kufa papo hapo siku
hiyo saa 1:30 jioni.
Alisema wakati wakiupakia mwili huo kwenye gari
la polisi namba PT 1424 huku likiwa limeegeshwa pembeni mwa barabara,
basi hilo lilitokea ghafla kwa kasi na kuwagonga watu 15 na kufariki
dunia papo hapo, wengine wanne walikata roho wakati wakipelekwa
hospitalini.
Kamanda Kamwela alisema dereva wa basi hilo, Paulo
Njilo, mkazi wa jijini Dar es Salaam baada ya kukaribia eneo hilo
aliliona gari la polisi likiwa limeegeshwa pembeni kushoto mwa barabara,
lakini wakati akijaribu kulikwepa ndipo alipoliparamia kundi la watu
waliokuwa na askari.
Aidha, alisema dereva wa basi hilo baada ya
ajali hiyo aliendelea na mwendo hadi aliposimama kilomita 25 katika
makao makuu ya Wilaya ya Ikungi na kutokomea kusikojulikana, lakini
juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Kamanda huyo aliwataja askari
waliokufa kuwa ni F.849 D/CPL Boniface Magubika wa CID Wilaya ya
Singida, F.6837 Pc Jumanne Mwakihaba wa FFU Singida, G.7993 Pc, Novatus
Tarimo wa ofisi ya RCO na G.8948 Pc, Michael Mwakihaba wa FFU Singida.
Wengine
ni Ofisa Mtendaji Kijiji cha Utaho, Ramadhan Mjengi; Mwenyekiti wa
Kijiji Utaho, Paul Hamis; Mwenyekiti wa Kitongoji cha Utaho, Ernest
Salanga; Said Rajab, Usirika Itambu, Chima Mughenyi, Salim Juma, Abeid
Ramadhan, Mwinyi Hamis na Issa Hussein, wote wakazi wa kijiji cha Utaho.
Kamanda
Kamwela alisema miili ya marehemu wengine wanne bado haijatambuliwa na
ndugu zao na imehifadhiwa kwenye chumba cha maiti katika Hospitali ya
Mkoa wa Singida.
Kamanda Kamwela alisema majeruhi wawili kati ya nane
wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa Singida na wengine
sita wapo hospitali ya Misheni Malikia wa Ulimwengu iliyopo Puma.
Aliongeza
kuwa miili ya askari polisi inatarajiwa kusafirishwa kwenda katika
mikoa wanakotoka wakati wowote baada ya taratibu za kipolisi kukamilika
ikiwamo kuwasiliana na ndugu zao walioko mikoa ya Kilimanjaro, Pwani,
Mbeya na Iringa


Comments
Post a Comment