MAREKANI NA UMOJA WA MATAIFA WALAANI MASHAMBULIO YA GAZA.

Marekani na Umoja wa Mataifa wamelaani mashambulio dhidi ya raia waliokuwa wamekimbilia katika shule moja Gaza.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema shambulio hilo, lililosababisha vifo vya watu 16 ni "uovu". Israel imesema jeshi lake lilikuwa likijibu mashambulizi yaliyokuwa yakitokea karibu na shule hiyo.
Zaidi ya watu 100 wameuawa Gaza siku ya Jumatano, wamesema maafisa wa Palestina. 
Mashambulio katika soko lililopo karibu na Gaza lilisababisha mauaji ya watu 17, huku mitego ikisababisha vifo vya waisraeli watatu.
Madaktari wa Palestina wamesema shambulio la anga la Israel lilisababisha vifo vya watu saba katika mji wa Khan Younis.
Wizara ya afya ya Gaza imesema watu 106 waliuawa siku ya Jumatano, na kufikishwa jumla ya raia waliouawa mpaka sasa kufikia 1,336.
Watu 58 wa Israel wameuawa 56 kati yao wakiwa wanajeshi na raia wawili.

Comments