NEWS ALERT!! LADY JAY DEE KUWASILI DAR AUGUST 3 NA TUZO YA AFRIMMA.

Anaconda, Lady Jay Dee ambaye ameshinda tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki atatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, August 3 mwaka huu akitokea Marekani.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, meneja wa Lady Jay Dee, Captain Gardener G. Habash amesema kuwa mwimbaji huyo anatarajia kuondoka Houston, Marekani August 1 na kuingia Dar es Salaam August 3.

Amesema Lady Jay Dee yuko Marekani alikuwa ameenda kwa ajili ya likizo au mapumziko.

Tuzo hiyo ya AFRIMMA imekuwa tuzo ya 30 kwa muimbaji huyo, idadi hiyo ilifahamika rasmi baada ya kuandika ujumbe wa shukurani kwa mashabiki wake.

Source: Times

Comments

  1. mbona unachanganya watu,anatua dar august 31,then manager kasema anaondoka houston tarehe 1 nakufika dar tarehe 3.so which is which.

    ReplyDelete

Post a Comment