Wiziri ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemkingia kifua msanii wa sanaa ya maigizo kutoka Tanzania Amir Athuman a.k.a King Majuto/Mzee Majuto dhidi ya kampuni inayomzungusha juu malipo yake ka kazi za sanaa zenye thamani ya milioni 25 ndani ya miaka miwili.
Akizungumza na wadau wa sanaa wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika tarehe 27 katika Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe ameonesha kuguswa zaidi na hali na muigizaji King Majuto kunyanyasika kwa kukosa haki yake hata kuhaidi kuwa yuko tayari kulivalia njuga hilo hata kuutumia mshahara wake pale itakapobidi ili kufanikisha malipo hayo ya King Majuto.
Comments
Post a Comment