Linah Sanga amesema hana mpango wa kuwa producer licha ya kuwa mmiliki wa studio yake mwenyewe ya Drop Out Entertaiment.
Ameiambia Dizzim Online, “Mimi ninachoamini kwenye fani hii kama muimbaji basi imba kwasababu huwezi kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja, yaani kuimba na kuproduce lazima sehemu moja utaraharibu tu. Kwasababu utajikuta mwisho wa siku unaegemea sehemu moja, so mimi sifikirii kuwa producer, mimi nataka kuimba basi.”
Hivi karibuni Linah alijaaliwa kupata mtoto wa kike na bado amekuwa kimya kwenye muziki.

Comments
Post a Comment