Na Evance Ng'ingo
MWANAMITINDO wa kimataifa afanyaye shughuli zake
nchini Marekani, Flaviana Matata madarasa mawili ya shule za msingi iliyopo
katika kijiji cha Msinune kilichopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani.
Flaviana alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na
wanakijiji wa Msinune mwaka 2014 wakati alipoenda kuwasaidia wanafunzi mabegi ya
shule, walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja
na kumalizia ujenzi wa darasa.
Tangia alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa
vyoo vya walimu na wanafunzi, na juzi alienda kukabidhi jengo la madarasa,
darasa la saba na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Flaviana
alisema, tangia alipopewa jukumu la ulezi wa shule hiyo amekuwa akihangaika
huku na kule kupata fedha za kutatua kero za shule hiyo.
Alisema, kwa kufanikiwa kukabidhi jengo hio la
madarasa anaona kuwa ameshiriki kikamilifu katika kutekeleza jukumu lake kama
mwanajamii la kusaidia maendeleo ya elimu kwa jamii iliyokuwa na uhitaji
mkubwa.
Alisema" sisi kama vijana kama watanzania
tunalo jukumu la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine
muhimu nchini kwa kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake, sasa
nimeshatengeneza vyoo vya walimu na wanafunzi na leo nakabidhi darasa"
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Alex
Lugaigalila alisema ujenzi wa darasa huo utawaongezea ufanisi wanafunzi katika
masomo yao huku akibainisha wazi ushiriki wa Flaviana kwenye maendeleo ya shule
hiyo umeongeza hamasa ya wanafunzi kusoma.
Kwa upande wake Afisa wa elimu wa Kata hiyo,Blasius
Alphonce alisema kwa ujenzi wa jengo hilo, Flaviana amesaidia jitihada za serikali
katika kuendeleza elimu kwenye kata hiyo yenye vijiji vitano.
Jengo hilo la darasa lililojengwa lina vyumba viwili
vikubwa vilivyoezekwa kwa bati huku likuwa na madirisha makubwa yanayowezesha
kupitisha hewa na chumba cha mwalimu mkuu.
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake
nchini Marekani, Flaviana Matata (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa jengo alilojenga la madarasa mawili na ofisi ya mwalimu mkuu wa
shule ya msingi kwa shule ya msingi Msinune, iliyopo kata ya Kiwangwa wilayani
Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini
Marekani, Flaviana Matata kushoto akikabidhi mipira kwa wanaafunzi wa shule
hiyo, Flaviana ni mlezi wa shule hiyo.
Mwanamitindo Flaviana akionesha cheti cha heshima
alichotunukiwa na uongozi wa kata ya Chiwangwa baada ya kuwajengea majengo ya
shule.
Flaviana akipokea zawadi ya mbuzi kutokea kwa
Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhan Mtokeni (kushoto) huku Diwana wa
kata ya Chiwangwa (kulia) Malota Kwagga na Afisa elimu wa kata hiyo Blasius
Alphonce kulia kwa diwani na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msinune, Alex
Lugaigalila wakiangalia.
Flaviana akiwahoji wanafunzi hao maendeleo yao ya
masomo shuleni hapo.
Flaviana akiwa amekalia moja kati madawati 45 ambayo
aliyatoa kwa shule hiyo mwaka jana, kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi
Msinune, Alex Lugaigalila na kushoto ni Afisa elimu wa kata hiyo Blasius
Alphonce.
Flaviana akipokea cheti cha heshima kutokea kwa
Mtendaji wa Kijiji cha Msinune, Memory Mbangwa cha kutambua mchango wake huo.
Flaviana akiwa na watendaji wa kijiji hicho na kata
pamoja na wanakijiji waliojitokeza siku
hiyo.
Alipata wasaha wa kupiga picha na wanafunzi pia siku hiyo ambao walimpongeza
kwa msaada wake huo
Comments
Post a Comment