Mrembo Hamissa Mobetto anaonekana kuwa anazidi kushindilia msumari wa moto juu ya uwezekano wa kuwa ana ukaribu zaidi na baba ‘Prince Abdul’ kwa kuweka picha tofauti zinazohisiwa moja kwa moja kuwa yuko katika mahusiano na mzazi mwenzake huyo, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz.
Siku za hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Snapchat aliweka picha iliyoonesha miguu yake na miguu ya mwanaume na kuandikwa ‘Bae & I…Looooove his Shoe” na aliyehisiwa kuwa ni yeye na Diamond Platnumz na viatu vilivyoonekana katika picha ni vile vilivyoonekana katika video ya #Kwangwaru.
Mara hii Hamisa ameweka picha ya mkono wake ukiwa umeshikana mkono wa mwanume ambaye tena amehisiwa ni Diamond Platnumz na kuandika “Diamonds ain’t nothing when I’m shining with ya Love” na hapa bado waliowengi wanazidi kuamini kuwa hisia za penzi zito zinawezekana kuwa zinatanda kati yao kutokana na dalili ya vinavyozidi kuonekana kwa upande wa Hamisa.
story dizzmonline
Comments
Post a Comment