Faiza Ally ''ushirikaino wa bongo movie kwenye Mazishi ya Agenes Masogange Uwepo hadi kwenye Kaziwatapiga hatua kubwa ''
Msanii wa Bongo Movie na mjasiriamali Faiza Ally amesema jambo kwenye ukurasa wake wa Instargram kwamba Bongo Movie wameonyesha ushiriano mkubwa kwenye msiba wa Agness na huku akiwapongeza watu kama Irene Uwoya ,Zamaradi Mketema na wengine wengi kwa kusimama imara katika kipindi cha Msiba wa Agnes Magogange.
Aliendelea kwa kusema kwamba Bongo Movie wana vitu vikubwa sana lakini hajui wanakosea wapi ,akiamini kwamba ushirikiano walio onyesha kwenye msiba wangeupeleka kwenye kazi zao watapiga hatua kubwa sana
Tunaishi kwa kujifunza na mara nyingi mitazamo ya nje sio halisi, naomba nimpongeze @ireneuwoya8 kwa kuwa rafiki mwema a special kipindi hiki , nimemuona akishiriki na kwenye utulivu sana yaani kasimama kama rafiki na hivi ndio inavyo takiwa , yaani jambo linapo kufika la mtu wa karibu sio kulia sana au kupoteza fahamu lzm usimame ujue hatma ya mwenzio kwanza, nampongeza sana @zamaradimketema@stevenyerere2 @auntyezekiel@official__husnamaulid_ @husnasajent_@shilolekiuno_badgirlshishi@chandeshian_homeaccesories na wengine ambao sikuweza kuwataja kwa kweli mmesimama imara sana , nahisi bongo movie tuna vitu vikubwa sana wote kwa pamoja lkn sijui tunakosea wapi, maana kwa ushirikiano huo huo wa msibani , urudi kwenye kwenye kazi naamini kuna hatua kubwa sana tutapiga ..nisema tu mpo vizuri sana ...... nyinyi ni wa maana sana , uwepo wenu ni muhimu M.MUNGU AWATUNZE 🙏
Comments
Post a Comment