''Kuitwa Mama Sio lazima uzae '' Mjasiriamali Maznatbridal Ampa Maneno ya faraja Wema Sepetu




Hakuna mtu ambaye hajui kwamba Wema Sepetu anapenda sana na kutamani kuitwa Mama,amekua aki struggle a lot ,its heart breaking.
Mjasiriamali na influencer Maza Sinare aka Maznat Bridal amemfariji Wema kwa Maneno haya ya faraja.


Kuitwa mama siyo lazima uzae. Ukifikia umri tu wa kuitwa aunt, mama mdogo, shangazi, mama mkubwa ina maana wewe tayari ni mama. Kuwa mama siyo lazima uingie labour, mimi namshukuru Mungu nimezaa na nimelea watoto wangu na wasio wangu...na katika yote nimejifunza KUPENDA WATOTO KWA DHATI PASIPO KUBAGUA. Nimejifunza UKIWAPENDA upendo wa kweli huwa wanajua na wao WATAKUPENDA HIVYOHIVYO. Lakini zaidi nimeshawahi penda watoto yatima na kujitoa shilingi yangu ya mwisho kuwahudumia angali sikuwahi kuwaona wazazi wao. Tena nikawapenda kwa moyo wangu wote na nguvu zangu zote na wala sikuwa nimewazaa. Mungu ni msiri sana sana mdogo wangu @wemasepetu anajua nini kinamstahili nani, kwa muda gani. Muda wa Mungu ukifika ataku suprise. Atakupa faraja ya ajabu. Atakupa kile moyo wako unahitaji. Atakutunuku zawadi ya kipekee...utabaki mdomo wazi...ukishangaa maajabu ya Muumba. Jipe moyo. It is well. Eeeh Mungu, kila mwanamke apate katotoo angalau kamoja... Amina. 🙏🙏 mlale unono. #maznat #maznatbridal #badilimtazamo#amkanamaznat ( nimemuwaza sana Aggy na mtoto wake...nikamuwaza sana Wema. Roho imeniuma...nakuombea sana Wema upate ka kwako Inshaalah🙏🙏🙏)

Comments