Romy Aonyesha Ukomavu Awaomba Radhi Barakah The Prince na Naj

Romy Jons ni Dj na anafanya kazi na Diamond Platnumz ,ameonyesha maturity sana kwenye hili na amewaomba msamaha Barakah The Prince na mpenzi wake Naj kwa yale yaliyojitokeza siku chache zilizopita.

Romy alikua na tuhuma nzito za  Naj kupitia DM ya Instagram huku akimtolea maneno ya kashfa Barakah huku akimsifia Naj

Dj huyo ameowaomba radhi wawili hao kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika
NICHUKUE FURSA HII KUMUOMBA RADHI MSHKAJI,RAFIKI,NDUGU YEYE PAMOJA NA MPENZI WAKE KAMA NIMEWAKWAZA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE,NISINGEPENDA HAYA MALUMBANO YAENDELEE KWA SISI KAMA VIJANA INATUPASA TUKAE TUPANGE TUNAWEZAJE KUJIKWAMUA NA HUU UMASIKINI NA SANAA YETU KWA UJUMLA!!!!PIA NIOMBE RADHI KWA FAMILIA YANGU,NDUGU ZANGU,MARAFIKI ZANGU NA MASHABIKI ZANGU KWA UJUMLA KWA LOLOTE LILILOJITOKEZA!!! MUNGU ATUONDOLEE UADUI NA TUENDELEE KUFANYA KAZI INSHAALLAH
Vile vile  jana pia Romy alimuomba msamaha mkewe kutokana na tukio hilo ambalo lilionekana kuelekea kuvunja ndoa yake

Comments