Shule ya Msing Msinune yakabidhiwa mradi wa maji safi na salama kutoka kwa Flaviana Matata Foundation na Tasha Oakley
Ukosekanaji wa maji safi na Salama ni moja ya vitu vinavyo athiri upatikanaji wa elimu bora.
Leo kwa kushirikiana na Natasha Oakley tumekabidhi rasmi mradi wa maji safi na salama wenye hifadhi ya maji ya lita 32,000 kwa matumizi ya wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Msinune.
Vilevile tumekamilisha ukarabati wa madarasa saba (7), ofisi za walimu mbili (2) na maktaba.
Changamoto iliyobaki shuleni hapo ni ujenzi wa nyumba 10 za walimu ambazo tunaamini tutazikamilisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya elimu. Asanteni wote kwa ushirikiano wenu.
Comments
Post a Comment