Shamasa For amewashukia watu ambao wanasaidia wenzao kwenye maisha lakini wanajisahau na kuishia kujiona miungu watu na kutaka kusujudiwa kisa tu wamekusaidia na kama haitoshi wanakutangazia na kukusimanga ,kukuonyeha kwamba bila wao huwezi kuishi .
Alipost ujumbe huu kwenye page yake ya instagram
kila mtu anapenda kusaidiwa lakini kuna misaada mingine mpaka mtu unajuta kwann umesaidiwa. utafanywa tangazo kila sehemu,utasemwa na kusimangwa kila sehemu,utafanywa mtumwa,hata kama akikuudhi itabidi tu umchekee, Huyo mtoa msaada atajiona Mungu MTU kwamba bila YEYE maisha hayaendi, hapo bado hajakubania sehemu utasema yeye ndo mtoa RIZIKI. Misaada ya aina hiyo ni bora ikupite ufe na shida zako tu maana itafika sehemu utamsujudu yeye na kumsahau Mwenyezi Mungu ..
Comments
Post a Comment