Diamond Platnumz asema watu wasimletee u team kwenye watoto wake,Amuita Dylan ''My beloved kid''

Diamond platnumz amewatolea uvivu watu wenye team zao ambao wanasema anambagua mtoto wake Dylan sababu tu hakua kwenye video ambayo watoto wake wengine Nillan na Tiffah walikuwemo.

Asema wala hawabagui wote ni watoto wake 
“His is my Kid and he will forever be my Kid, tena My Beloved Kid, na si vinginevyo. Halafu cha kuongeza, msiniletee U-team wenu kwa watoto wangu! they are all my Kids, Nawapenda na siwezi mtenga wala kumbagua yeyote,” ameeleza Diamond.
Diamond Platnumz ni baba wa watoto watatu, watoto wawili ‘Tiffah na Nillan’ akiwa amezaa na Zari The Boss Lady na mtoto wa mwisho, Daylan akiwa amezaa na Hamisa Mobetto.
Kufuatia kitendo cha Hamisa Mobetto kuzaa na Diamond wakati muimbaji huyo bado alikuwa na mahusiano na Zari ndicho kilipelekea warembo hao kuanza kurushiana maneno mitandaoni kitu kilichokuja kuzaa kile kinachoitwa team Hamisa na team Zari.

Comments