Wizara ya mifugo na Uvuvi imemtoza faini ya Shilingi laki tatu mmiliki wa mgahawa wa Bunge Daniel Lamba baada ya kukamata samaki wadogo aina ya sato wanaodaiwa wamevuliwa kinyume cha sheria. Samaki hao walikuwa tayari kwa ajili ya kuliwa.
Naibu Spika Dr Tulia Ackson ametoa maagizo kwa Serikali hadi kufikia kesho kesho iwe imewasilisha Bungeni taarifa kamili kuhusiana na tukio la maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanaodaiwa kuingia katika canteen ya viwanja vya Bunge na kupima samaki waliodai kuwa hawajakizi vigezo vya kuvuliwa.
Comments
Post a Comment