Gigy sijamsikia nna muda mambo yamekua mengi insta kukeep track ya kiki inaanza kua ngumu,Anyway mwimbaji wa bongo Flava Gigy money anaetamba kwa sasa na wimbo wake wa Kiki na Gigy
Gigy ameiambia Enewz ya EATV kwamba, haiwezi ikatokea mtoto akawa na role model tofauti na mtu ambaye amemzaa.
“Kila mtoto yoyote ‘role model’ wake ni mama yake mzazi hata iwaje. Uwezi kusema mwanao atakuwa ‘role model’ wa mtu mwingine. Hivyo mwanangu atakuwa tu vyovyote atakavyotaka kuwa mimi nitampa ushirikiano. siwezi kumlaumu hata akitaka kuwa kama mimi ila ndio ntazidi kufurahi”, amesema Gigy.
Pamoja na hayo, Gigy ameendelea kwa kusema “siwezi kujutia kuzaa halafu kingine ni kwamba kujipanga utajipanga baada huko wala hupaswi kuwaza kuwa itakuaje nikifanya jambo fulani. Maisha ya siku hizi hayana hiyo kitu, Mungu yupo kila siku anatenda”
Comments
Post a Comment