Zamaradi Mketema Awashushia Waraka Mzito walisema Alichangisha watu kwenye 40 ya Mtoto wake ,Wachawi watajwa

Kablaya 40 ya mtoto wake wa 3 King Salah watu walisema anachangisha kufanya sherehe akawa amepinga swala hilo,ila wabongo being wabongo hawakulimaliza hili swala waliendelea kuongea mengi,Zamaradi jana akaona atoe ufafanuzi kuanzia kutokushona nguo kwa Hamisa Mobetto Mobetto Styles mpaka yeye kusema anaharibiwa brand yake ndo maana ameona aseme.

PART 1.

Imenilazimu niongee haya kwa minajili ya kulinda BRAND YANGU na watu NILIOINGIA NAO MKATABA KWASASA hivyo mniwie radhi nitaowakwaza.

Zamani wachawi walikuwa wanajificha wanasubiri giza liingie wapae, ila siku hizi wachawi wamehamia INSTAGRAM wazi kabisa, wanapoona kuna MAFANIKIO, HESHIMA ama MAPENZI kwako watatafuta kila sababu ya KUKUSHUSHA NA KUKURUDISHA CHINI MAKUSUDI kwa kutafuta na kutunga UONGO NA UZUSHI bila uoga wala haya ya kuona wanaongopa, lengo ni kukushusha mfanane, nataka niseme HATUTAFANANA!! Na nimeamua kuongea maana hata UONGO UKINYAMANZIWA SANA HUAMINIKA.



baada ya 40 ya mwanangu kupita, kuna wapuuzi wenye chuki wamejitokeza na kuanza kusema mimi nimechangisha hela ya kufanya 40, na ni kitu kinachosambazwa kwa kasi mno na kutaka kuaminishwa kwa nguvu mpaka inakwaza sasa kiubinaadamu, hivi hii inaingia akilini!!?? kwanza kabisa huo sio utaratibu wangu na kwangu hilo ni swala la aibu sababu sherehe kama ya 40 ni HIARI sio kitu cha lazima, mwanzoni walisema nimechangiwa na wanakamati kutokana na group la rafiki zangu kwa mapenzi yao kujikusanya kuninunulia ZAWADI YA SURPRISE ambayo ni SETI YA 
DHAHABU waliyonikabidhi siku ya sherehe,

 tena sikujua hiko maana hata kwenye group walinitoa ili iwe surprise kwangu, na lengo la group mwanzo ilikuwa ni SARE ila baadae wakanitafutia zawadi kwa mapenzi yao kwangu na jinsi TUNAVYOISHI, ila hakuna mwanakamati wala mtu baki hata mmoja aliewahi kunipa hata SHILINGI MIA kama mchango kwangu au kunilipia chochote na SIJAWAHI KUOMBA sababu sio utaratibu wangu na kwenye lile NILIJITOSHELEZA, hivi mmeshindwa kutofautisha ZAWADI NA MICHANGO!?? Sababu tu ya kuona wenzangu wana mapenzi kiasi gani na mimi kuna wengine wanaumia tu na wanabadilisha mada kuwa nimechangiwa, kweli!?? Kama niliweza kufanya EVENT ya wanawake wenzangu BURE iliyonicost sio chini ya MILIONI NANE tena bila kusaidiwa na mtu YOYOTE kwa mapenzi tu na kutoa elimu na hawakulipa viingilio leo iweje nichangishe!?? Sio kila mtu ANAPENDA KUJISHAUA NA KUONGEA AMA KURINGISHIA, tusilazimishane tabia zisizo zetu, na nime



INAENDELEA
PART 2.

Sio kila mtu ANAPENDA KUJISHAUA NA KUONGEA AMA KURINGISHIA, tusilazimishane tabia zisizo zetu, na nimeongea haya ili tu KULINDA BRAND YANGU inayotafutwa na watu kwa nguvu kutaka kuichafua baada ya maisha yao kuwashinda. 
Narudia tena Naongea yote haya not because nataka KURINGISHIA/BRAGGING but because IAM A BRAND, shughuli nzima kabla haijafanyika ilikuwa SPONSORED KILA KITU ULICHOKIONA, HAKUNA ALIENICHANGIA SUMNI YA 40 labda zawadi ambazo zilitoka kwao wenyewe kwa mapenzi yao wenyewe,ukinuliza zimekujaje sijui maana sikuwepo kwenye group zao kujua mipango yao ila naamini ni UTU WAO KWANGU.



Wameona imepita wanaanza kusema kuhusu group nyingine ya watu wa wonder women imenichangia, guys sikumuomba mtu zawadi, wala sijawahi kupiga tarumbeta kusema nataka mtu afanye kitu, watu wamejichanga wenyewe kuninunulia zawadi tena sidhani kama ilizidi elfu 80 tu za KITANZANIA kwa hilo group linalosemwa la watu sio chini ya 200 ambao kwa pamoja ndio hiyo elfu themanini, sikujua wamepanga saa ngapi wala sikuomba bado naamini ni UTU WAO, kweli sherehe ya sio chini ya MILIONI 20 useme nimechangiwa kupitia hiyo hela ISIYOZIDI LAKI, ukiangalia kuanzia DECOR ambayo @partyboxevents amehusika sio chini ya milioni kumi (invoice attached) chakula, vinywaji, nguo, na kila unachokiona HAKUNA ALIETOA SHILINGI YAKE, tukija kwenye nguo naambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine!! Funny wallah!! Na nimeshangazwa sana na uongo mkubwa wa namna hii, Nimeattach ushahidi hapo juu kuwa MIMI NDIO NIMETUMA HUO MSHONO KWAKE NA SIO YEYE, hakuwa anaufahamu kabla, hata kama kuna roho mbaya mnanipa sio ya kiasi hiko, sasa hapo nani mbaya!? Kutokana na kupishana na muda nikaona nikashone kwingine, na zaidi Swala la kushona popote ni uamuzi, since sio mshono niliochukua kwa mtu nina uhuru wa kuupeleka popote, nina biashara ya duka la nguo nina CATERING ila silazimishi kila ananenijua aje kwangu, na zaidi SIJISIKII VIBAYA riziki inapoenda kwa wengine, sina roho mbaya hiyo, riziki kugawana. Am very dissapointed kiukweli na binaadamu ila nimegundua kinachofanya haya yote sio kwamba wananihofia mimi ila NGUVU YANGU. hata ukinyamanza kimya watu


INAENDELEA


Hata ukinyamanza kimya watu watalazimisha ubrag tu hata kama sio tabia yako, kuanzia kila ulichokiona hakuna nilichochangiwa wala kupewa bure, MSIMCHAFUE SPONSOR WANGU ambayo mimi ni BALOZI WAKE, watu walikula, walikunywa na na narudia tena NI PESA YA MFUKONI MWANGU iliyotokana na MDHAMINI WANGU.. ALINILIPA ZAIDI YA HIYO NA ACOCOVER COST ZOTE, Na naongea hivi pia kuprotect BRAND ya wadhamini wangu sababu uongo unapitiliza sana, nataka niseme hivi KWA KUJIAMINI. Sijawahi kuomba mchango, kuchangisha wala Kuchangiwa na yeyote kwenye 40 ya mwanangu, na zaidi kama kuna mtu angetaka kunichangia NINGEKATAA bado maana sioni sababu kwenye kitu kama cha kujifurahisha mwenyewe, leo natungiwa maneno kila kona ili tu kunishusha, nawahakikishia SITASHUKA KWA HILO, na zaidi yeyote alieleta chochote kutoka popote ni ZAWADI AMBAZO SIKUOMBA ila mapenzi ya watu binafsi, sina shilingi kumi ya mtu niliyokula na HAKUKUWA NA HELA YA KULIWA inayoweza kunisaidia kwenye party wala maisha yangu, nawaruhusu kunichukia ila msilazimishe uongo kuwa kweli, kuna tofauti kubwa kati ya ZAWADI NA MICHANGO hivi mimi nina power gani ya kulazimisha watu wachange na wakachanga kwa kuniogopa, hivi NINAOGOPEWA KIASI HIKO ama NINA NGUVU HIYO!?? Au kuna karama mnayoiona ambayo mimi sijaigundua!?? Kweli jamani!??? Aaaaaah msifanye hivyo, kuna muda kubali yaishe, ZAMU YANGU IMEFIKA.. badala ya kukalia majungu na roho mbaya muombe MUNGU akuone, usiwe busy kushusha watu kwa uongo na uzushi na kuwachafua ama kuwatukanisha HAITAKUPANDISHA WEWE!! Sana sana unajibebea laana za kushindwa kuendelea, hata MBELE ZA MUNGU hafurahii.

Nisameheni niliowakwaza, nililazimika kuliweka hili sawa sababu lilitaka kuathiri hadi brand ya wengine ninayoisimamia mimi.

MNIWIE RADHI.

Comments