Yaliyozungumzwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini

Wito umetolewa kwa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuongeza jitihada katika kusimamia viwango vya usalama na afya katika sehemu za kazi ili kuwezesha utekelezaji wa sera ya serikali ya uchumi wa viwanda kuwa na tija zaidi.


Wito huo umetolewa na Jukwaa la Wahariri (TEF) wakati wa kikao kazi baina yao na menejimenti ya OSHA kilichofanyika katika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao kazi hicho, Katibu wa TEF, Nevelle Meena, amesema OSHA ina nafasi kubwa katika kulinda afya za wafanyakazi katika sekta ya umma, sekta binafsi pamoja sekta isiyo rasmi hivyo ni muhimu kwa taasisi hiyo kuhakikisha kwamba jamii ina uelewa wa kutosha kuhusu afya na usalama wao wawapo kazini.
Naye Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema lengo la kikao hicho ilikuwa ni kubadilishana uzoefu na kuwafahamisha wahariri kuhusu namna ambavyo OSHA inatekeleza majukumu yake ili kufanikisha suala zima la kuuelimisha umma kuhusu masuala ya usalama na afya katika sehemu za kazi hususani kuelekea uchumi wa Viwanda.
credit;Bongo5

Comments