BALOZI MAJAAR ATELIWA MWENYEKITI WA BARAZA LA CHUO KIKUU UDSM

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya Jaji mstaafu, Damian Lubuva aliyemaliza muda wake.

Pia, amemteua Prof. William Andey Lazaro Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa Muhula wa Pili.




Source: Ikulu Mawasiliano

#Zurii #ZuriiAfrica #Uteuzi #Tanzania

Comments