BIDHAA ZINAZOTENGENEZWA TANZANIA KUINGIA BILA USHURU UINGEREZA 2023

Zaidi ya Asilimia 99 ya jumla ya bidhaa ambazo zitasafirishwa kutoka Tanzania kwenda Uingereza zitaingia bila ushuru kuanzia 2023.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania ameeleza kuwa kuwa bidhaa ambazo zitapewa kibali cha kuingia Uingereza bila ushuru ni zili zinazotengenezwa Tanzania tu. Pia alikazia kuwa vigezo hivi vitahusisha pia bidhaa zinazotengezwa kwa malighafi kutoka nchi zingine.

Hivi karibuni serikali ya Uingereza imezindua mpango mpya wa kibiashara na nchi zinazoendelea utakaoanza kufanya kazi mwaka 2023.

Comments