Martha Kara ambaye alikuwa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Azimio la Umoja katika Uchaguzi Mkuu 2022 amesema kazi haijamalizika na kuna uwezekano wa kumpa changamoto Rais Mteule William Ruto
Karua hajafafanua kuhusu kauli yake hiyo ikiwa ni wakati ambao Raila Odinga bado hajatoa tamko lolote hadi kufikia saa 12:50 Asubuhi leo Agosti 16, 2022.
Kabla ya matangazo ya ushindi wa Ruto, Tume Huru a Uchaguzi iligawanyika kuhusu matokeo hayo.
Kanuni za Uchaguzi zinaruhusu kupinga matokeo Mahakama Kuu ndani ya siku 7 tangu kutangazwa kisha Mahakama Kuu nayo inatakiwa kutoa majibu ndani ya siku 14 tangu kufunguliwa kwa shauri.
#KenyaDecides2022 #Democracy #Kenya2022
Source: Jamii Forums
Comments
Post a Comment