Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania - Taifa Stars kupoteza kwa kufungwa 1-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu CHAN, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kumuondoa Kocha Mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen Raia wa Denmark pamoja na Wasaidizi wake.
Poulsen anaondoka katika nafasi ya Ukocha Mkuu Taifa Stars na kusalia katika Timu za Vijana hadi mkataba wake utakapomalizika, nafasi ya Kim itachukuliwa na Hanour Janza, akisaidiwa na Meck Mexime huku Juma Kaseja akiwa Kocha wa Magolikipa.
Source: TFF
Comments
Post a Comment