Wakati sense ya Watu na Makazi ikiendelea nchini, makarani wawili wamejikuta katika wakati mgumu baada kuporwa vifaa vyao vya kukusanyia taarifa maarufu kama vishikwambi na vibaka.
Tukio la kwanza limetokea jijini Arusha ambapo karani aliyetambuliwa kwa jina la Saraphia Kiwango ameporwa kishikwambi chake alipokuwa akielekea kuanza kuhesabu makundi maalum katika Kata ya Unga Ltd.Katika halmashauri ya Mpimbwe kata ya Majimoto mkoani Katavi, karani aliyetajwa kwa jina la Kenani Kasekwa amevamiwa na mtu asiyejulikana na kumwibia kishikwambi na fedha taslimu Sh760,000
Comments
Post a Comment