Marubani wasimamishwa kazi kwa kupigana wakiwa angani

Shirika la Ndege la Ufaransa, limewasimamisha kazi marubani wake wawili wa Air-France kwa kupigana wakati wakirusha Ndege ya Airbus A320 kutoka Geneva kwenda Paris Juni 2022

Wafanyakazi wengine waliingilia kati ugomvi baada ya kusikia kelele ambapo waliamua kuwatenganisha vyumba na rubani mmoja alirusha Ndege hiyo hadi ilipotua salama

Ripoti ya Bodi ya Shirika la Uchunguzi wa Anga la Ufaransa (BEA) ilionesha kuwa baadhi ya marubani wa Air France hawana ustaarabu na pia hawaheshimu Itifaki za Usalama.

Source: Jamii Forums

Comments