MBWANA SAMATTA KUREJEA GENK KWA MKOPO

Mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Ally Samatta amejiunga katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji akitokea Fenerbahçe ya Uturuki.

Amerejea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu kukiwa na uwezekano wa kumnunua, na tayari ametambulishwa Genk. Amenukuliwa akisema "Nimerudi".

Samatta alipata mafanikio makubwa alipoichezea Genk mwaka 2016 hadi 2020, baada ya hapo alijiunga na Aston Villa ya England.

Source: Jamii Forums

Comments