Mwanamke mmoja nchini Rwanda mwenye umri wa miaka 24 anashtakiwa kwa kosa la kuvaa vazi la aibu hadharani huku hukumu yake ikisemwa kuwa hadi miaka miwili gerezani.
Liliane Mugabekazi alikamatwa Agosti 7 ambapo picha zilimuonyesha akiwa amevalia vazi lilioonyesha sehemu za mwili wake alipohudhuria tamasha la msanii maarufu kutoka Ufaransa siku nane kabla.
“Alihudhuria tamasha huku akiwa amevalia nguo zinazoonyesha sehemu zake za siri… nguo ambazo tunaziita za aibu,” waendesha mashtaka walisema, wakimtuhumu kwa kufanya “uhalifu mkubwa”.
Habari za kukamatwa kwake zilizua hasira kwa baadhi ya Wanyarwanda, lakini maafisa wa serikali akiwemo waziri wa zamani wa sheria Johnston Busingye waliunga mkono hatua hiyo.
Serikali ya Rwanda imeweka sheria hii ili kulinda na kukomesha mmomonyoko wa maadili ambapo vitendo kama hivi vimeshamiri siku za hivi karibuni.
Comments
Post a Comment