Hart amepost kwenye ukurasa wake wa instagram ameandika "INATOKEA! Siku ya Alhamisi, Agosti 25, mgahawa wangu @myharthouse utafungua milango yake Los Angeles. Tunayo furaha kukuletea chakula cha haraka chenye ladha na bei nafuu. Nina shauku sana kwa kila mmoja wenu kuonja chakula chetu. Mambo yatakuwa moto wiki nzima, mtagi mtu wako aliye Los Angeles ambaye ungependa apate taarifa hii".
Aidha @myharthouse imeainisha kuwa 10% ya faida yatakayopatikana siku ya ufunguzi itatolewa kwa kituo cha Inner City Arts ambacho kinawasaidia watoto kupitia sanaa ya uchoraji.
Ikumbukwe kuwa miezi kadhaa iliyopita Hart alitambulisha kinywaji chake aina ya tequila kilichopewa jina Gran Coramino Tequila akishirikiana na Juan Domingo Beckmann kama muanzilishi mwenza.
Source: Kevin Hart - Instagram
Comments
Post a Comment