Mambo ni poa kabisa sasa kwa kila anayepanda Mlima Kilimanjaro kutoka na kuwepo na internet ya kasi iliyounganishwa hivi karibuni. Hii itawawezasha wapandaji kuweza kuwasiliana na familia pamoja na marafiki na kushea picha na video kupitia whatsapp, instagram, twitter, facebook na mitandao mingine ya kijamii wawapo juu ya Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Habari Nape Nnauye akilitaja tukio hilo kuwa la kihistoria. Baada ya kushiriki katika kusimika mtandao wa broadband unaomilikiwa na shirika la mawasiliano Tanzania - TTCL.
"Wageni wote wataunganishwa hadi sehemu hii ya mlima," alisema katika Vibanda vya Horombo, moja ya kambi zinazoelekea kileleni. Huku akikazia kuwa kilele cha mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 kitakuwa kimeunganishwa na mtandao wa intaneti ifikapo mwisho wa mwaka.
Comments
Post a Comment