Lewis Hamilton ameshindwa kuficha furaha yake alipokaa na watu wa Pokot nchini Kenya huku akiendelea 'kulitafuta chimbuko lake'.
Lewis mwanamichezo wa mbio maarufu za magari duniani Formula One ametumia muda wake wote wa likizo kulitafuta chimbuko lake barani Afrika.
Jumanne iliyopita aliweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram zilizoonyesha jinsi alivyofurahi kukutana na watu wa jamii ya Pokot nchini Kenya huku akionyesha kufurahishwa sana na jambo hilo.
Kati ya mambo yaliyofurahisha zaidi ni pale alipoonekana akicheza na mwanamke aliyevalia mavazi ya kiasili pamoja na mkufu wenye rangi mbalimbali na hereni.
Lewis aliandika 'Nimekutana na watu wa Pokot nchini Kenya na kuwa pamoja ilikuwa jambo moja... Kukaribishwa ilikuwa kitu tofauti kabisa na heshima kubwa siichukulii kirahisi.
Jinsi nilivyohisi hapa ndivyo ninavyohisi nikiwa na familia yangu nyumbani. Sisi sote ni familia. Nitalichukua tukio hili, na kumbukumbu zangu zingine zote kutoka Kenya na safari hii kwa ujumla, moyoni mwangu milele.
Source: MailOnline
Comments
Post a Comment