TANESCO: MABORESHO YA MFUMO WA LUKU YAAHIRISHWA

Shirika la umeme Tanzania 'TANESCO' jana lilitangaza kuahirisha zoezi la maboresho ya mfumo wa LUKU lililotangazwa siku ya tarehe 16 Agosti ambalo lilitegemewa kuchukua nafasi kati ya tarehe 18 hadi 21 Agosti. Ambapo yangepelekea kutokupatikana kwa huduma ya LUKU kwa tarehe hizo.

Hata hivyo siku ya jana TANESCO ilitangaza kuahirishwa kwa zoezi hilo hadi pale shirika litakapotoa taarifa ya kuendelea nalo.

Source: TANESCO

Comments