UPUNGUFU WA UMEME MIKOA 14

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limetangaza upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa 14 nchi nzima kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye moja ya mitambo ya kuzalishia umeme kwenye bwawa la Mtera.

Hitilafu hii imesababisha upungufu wa uzalishaji umeme na kupelekea kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Iringa, Manyara, Singida, Geita, Arusha, Morogoro, Shinyanga, Njombe, Tanga, Pwani na Dar es salaam.

TANESCO hawajataja ni siku gani huduma ya umeme itarejea kwenye hali yake ya kawaida lakini taarifa yao imesema "Wataalamu wetu wanaendelea na jitihada za kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa Wateja wote na tutawataarifu huduma itakaporejea, Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote ule unaojitokeza.

Source: Tanesco

Comments