Mchungaji Mpho Tutu van Furth azuiliwa kuongoza Ibaada ya Mazishi

Mchungaji Mpho Tutu van Furth ambaye ni Binti wa Marehemu Askofu Desmond Tutu, jana alizuiliwa na Kanisa la England kuongoza mazishi sababu ameoa mwanamke mwenzie.

Mpho alifunga ndoa na Marceline Desemba 2015 na alilazimishwa kuacha kufanya kazi kama Mchungaji nchini Afrika Kusini. 

Mwanamama huyo ni Mchungaji wa Dhehebu la Anglikana katika Dayosisi ya Washington na alikuwa akijiandaa kuongoza mazishi ya Marehemu baba yake wa kiroho. 

Binti Tutu aliliambia Shirika la habari la BBC kuwa "hali hii ni mbaya na inaumiza", huku dayosisi ikisema hii ni hali ngumu. 

Kanisa la England haliruhusu wachungaji wake kuwa kwenye ndoa za jinsia moja sababu mafundisho yake rasmi ni kuwa ndoa ni kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja. Hata hivyo Kanisa la Anglikana la Marekani linaruhusu suala hilo.

#zuriiafrica

Comments