Waziri wa Zamani wa China Anyongwa

Aliyekuwa Waziri wa Sheria wa China, Fu Zhenghua amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kupokea rushwa ya zaidi ya TZS Bilioni 65 akiwa mtumishi wa umma. 

Hukumu hiyo yaweza kutekelezwa ndani ya miaka miwili au kuwa kifungo cha maisha baada ya miaka miwili kumalizika.

Pamoja na hukumu hiyo, Zhenghua amefutwa uanachama katika chama tawala nchini China (CPC), ameondolewa haki ya kushiriki siasa za China maisha yake yote na mali zake zote zimetaifishwa.

#zuriiafrica 

Comments