Rais Samia kuunda kikosi kazi uratibu sera Nishati safi ya kupikia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa pendekezo la kuundwa kwa  kikosi kazi cha kitaifa kitakachoratibu dira na mwenendo wa kitaifa wa kuchakata sera na kuleta matokeo chanya ya kuwa na asilimia 90 ya watanzania watakaokuwa wakitumia Nishati safi ya kupikia katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Novemba 1, 2022 wakati akizindua mjadala wa kitaifa wa Nishati safi ya kupikia unaofanyika kwa siku mbili Novemba 1-2, 2022 ukilenga kujadili namna ya kumtua mama mzigo wa kuni kichwani na kuhamasisha matumizi ya gesi.

Amesema sehemu kubwa ya jamii nchini hasa maeneo ya Vijijini imekuwa ikikata miti kwa ajili ya kuni kutokana na bei ya mkaa kuwa chini na hivyo kuhimiza upandaji wa miti ya matunda ambayo wengi wao hawatoweza kuikata bila sababu ya msingi na kwafanya watumie nishati ya gesi kupikia.

Comments