*KAULI MBIU YA SHINDANO LA MWAKA HUU NI ‘UREMBO HALI’
Mkuu wa Udhamini wa Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, Bw. George Rwehumbiza akizungumza katika hafla fupi ya kuzindua rasmi shindano la Urembo la Vodacom Tanzania kwa mwaka 2011 wakiendelea kuwa wadhamini wakuu wa shindano hilo. Bw. Rwehumbiza alisema kwamba shindano la mwaka huu lina mvuto wa aina yake kwani warembo thelathini watakaoingia fainali hawataweka kambi hotelini kama ilivyozoeleka na watakaa kwenye nyumba maalum itakayojulikana kama nyumba ya Vodacom.
Kushoto ni Bw. George Rwehumbiza akipiga makofi pamoja na baadhi warembo waliowahi kushiriki wa Miss Tanzania kuashiria uzinduzi rasmi wa shindano la Miss Vodacom Tanzania 2011 pamoja na logo mpya ya shindano hilo. Kulia ni Mkuu wa Itifaki wa kamati ya maandalizi ya Miss Tanzania Bw. Albert Makoye na katikati ni warembo waliowahi kunyakua taji hilo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency pia Mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akitoa shukrani kwa wadhamini wakuu wa shindano la Miss Tanzania pamoja kuwatambulisha baadhi warembo waliowahi kushiriki wa shindano hilo.
Miss Tanzania 1997 Saida Kessy ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa akizungumza kwa niaba ya mamiss wenzake wakati wa uzinduzi huo.
Kutoka kushoto ni Miss Tanzania 2007 Richa Adhia, Miss Tanzania 2002 Angela Damas, Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim, Miss Tanzania 2000 Jacquiline Ntuyabaliwe pamoja na Miss Vodacom Tanzania 2010 Genevieve Mpangala.
Mwendesha shughuli MC Jokate Mwegelo akisherehesha.
Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza ( wa nne kushoto) katika picha ya pamoja na waratibu wa shindano la Miss Tanzania pamoja na warembo waliowahi kunyakua taji la Miss Tanzania.
Walioketi kutoka kushoto ni Mratibu wa Majaji wa kamati ya Miss Tanzania Dr. Ramesh Shah, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga, Mkuu wa Udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza, pamoja na Mkuu wa Itifaki ya Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye katika picha ya kumbukumbu na warembo mara baada ya uzinduzi.

Miss Tanzania 2007 Richa Adhia akiwa na mume wake mtarajiwa Hridhaan Dhillon.
Meneja Udhamini na Promotion wa Vodacom Bi. Rukia Mtingwa akimsikiliza kwa umakini Brother Ben Kisaka wa Jambo leo wakati wa kubadilishana mawazo katika hafla hiyo. Wengine ni Mkurugenzi wa T.H.T Ruge Mutahaba na Mkurugenzi Mtendaji wa Gazeti la Jambo leo na Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto.
Aba Billdard kutoka Vodacom akiwa na mdau katika pozi.
Warembo katika pozi
Mbunifu wa Mavazi Ally Rehmtullah akiwa na Warembo waliowahi kutwaa taji la Miss Tanzania.
Miss Vodacom Tanzania 2010 Genevieve Mpangala (kulia) katika pozi na balozi wa REDDS Consolata Lukosi
Wadau wakila wakinywa na kubadilishana mawazo katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam
Source & Image credits: MO BLOG
Comments
Post a Comment