.Wengi waguswa na Rais Kikwete
.Waimbaji wajifua kwa mashambulizi
Na Mwandishi Wetu
PASAKA ambayo ni kielelezo cha ushindi wa Yesu Kristo dhidi ya dhambi kupitia mateso, kifo na hatimaye ufufuko, imebisha hodi kwani itakuwa mwishoni mwa wiki hii. Wakristo duniani kote wamekuwa wakiiadhimisha Pasaka kwa maana ya kukumbuka fumbo la hili lenye maana kubwa kwa maisha ya kiroho kwa mkristo. Ni fumbo la kipee sababu, kwa kuteswa kwake Yesu pale Msalabani, wanadamu wakapata ukombozi.
Ndio maana Ijumaa ya wiki hii, itakuwa ni Kuu kwa maana na wakristo kukumbuka siku ya mateso na kufa kwa Yesu Kristo kabla ya kuushinda u-mauti alfajiri ya Jumapili.
Kiimani, kwa vile Ijumaa na Jumamosi, wakristo wote duniani watakuwa katika huzuni ya kifo cha Yestu Kristo, furaha yao itaanzia asubuhi ya Jumapili. Siku hiyo ya furaha kubwa kwa vile, baada ya Mariamu Magdalena na wengine kwenda makaburini, wakakuta jiwe limeviringishwa kando.
Wakiwa wamepigwa butwaa wakidhani mwili umeibwa, tazama alitokea malaika na kuwaaambia, mnayemtafuta amefufuka katika wafu na amewatangulia Galilaya. Kwa kutambua thamani ya Jumapili ya Pasaka yaani shangwe ya ufufuko wa Yesu Kristo (Aprili 24), Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, ikaamua kuisindikiza kwa furaha zaidi.
Kampuni hiyo chini ya Mkurugenzi wake Alex Msama, imeamua kuandaa Tamasha la Muziki wa injili ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee. Lengo la Tamasha hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa ni Rais Jakaya Kikwete, ni kuwaleta watu pamoja bila kujali tofauti za dini zao kwa sababu Mungu ni mmoja ili kupata burudani ya nyimbo za injili ambazo ni sehemu ya neno la Mungu.
Kwa upande wake Msama ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu Tamasha hilo, anasema maandalizi yaliyofanywa, ni ya kiwango cha kimataifa. “Hili ni tamasha la aina yake ambalo mabli ya maudhui yake ya kuwaleta watu pamoja kufurahia ushindi wa ufufuko wa Yesu Kristo, pia wengi watajifunza kitu kupitia mahubiri ya nyimbo. “Ndiyo maana Kamati yangu imejitahidi kuwashirikisha waimbaji kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kila atakayefika Diamondo, Jamhuri Dodoma na kule CCM Kirumba, Mwanza, arudi nyumbani akiwa ameshiba ujumbe wa neno la Mungu. ”Ukuu wa Mungu ni waajabu kabisa, mtu huweza kubadilika kiroho kupitia ujumbe wa neno la Mungu uliopo kwenye nyimbo za muziki wa injili, ndio maana hata Mkuu wan chi (Rais Kikwete), amekubali kuwa mgeni rasmi.
Msama anawataja waimbaji ambao watahudumu siku hiyo mbele ya Rais Kikwete, watanzani ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Mather Mwaipaja, Christina Shusho na Boniface Mwaitege. Kutioka nje ni Annastazia Mukabwa, Solomon Mukubwa, Pamela Wanderwa na Geraldine Odour kutoka nchini Kenya. Wengine ni Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayetamba na kibao cha ‘Hakuna Kama wewe’ na Ephraem Sekeleti kutoka Zambia.
Msama anasemaa anashukuru Mungu kwamba, mipango inakwenda vizuri na kilichobaki ni kuzidi kumwombea mgeni rasmi (Kikwete)afya njema siku hiyo afike Diamond Jubilee kuungana na wananchi kuifurahia Pasaka. Kwa upande wa waimbaji ambao watamba tamasha hilo, nao kwa nyakati tofauti kila mmoja amethibitisha kuwa katika maandalizi ya nguvu kwa ajili ya kufanya vitu vya uhakika.
Muhando kwa upande wake wanasema, yupo fiti na anazidi kumwomba Mwenyezi mungu azidi kumjalia uzima na afya ili siku hiyo yeye na waimbaji wengine, waweze kuisindikiza vizuti Pasaka.
Anasema, kwa vile Tamasha hilo litaanzia Diamond Jubilee kabla ya kuhamia Jamhuri Dodoma kisha CCM Kirumba, lile la Diamond Jubilee linapaswa kufunika zaidi.
KAULI ZA WADAU
Annastazia Ferdinand wa Kigilagila, jijini Dar es Salaam, anasema analisubiri kwa hamu kubwa tamasha hilo na anamwomba Mungu amjalie uzima na afya siku hiyo. “Nanalisubiri kwa hamu kubwa Tamasha la Pasaka nataka nikamwone Muhando (Rose), Mukabwa (Anastazia), kusema kweli wadada hawa wameimba vizuri sana kwenye albamu yao ya Kiatu,” alisema Annastazia au mama Catherine.
Mwingine aliyelizungumzia tamasha hilo, ni Vaileth Meshack ambaye mbali ya kutamani kwenda kwa ajili ya kuwaona live waimbaji mbalimbali, pia amekiri kuguswa na uwepo wa Rais Kikwete katika Tamasha hilo kama mgeni rasmi. “Niliposikia kwa mara ya kwanza kwamba Rais Kikwete ndie atakuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka sikiamini, jamani kumbe Tamasha linagusa wengi,” alisema Vaireth anayejiandaa kujiunga na Chuo cha Kilimo MATI Ilonga, Kilosa. Kingine kilichomgusa Vaileth katika tamasha hilo, ni hatua ya sehemu ya mapato ambayo yatapatikana, kuelekezwa kwenye makundi yenye shida kama yatima, wajane na waathirika wa Mabomu ya Gongo la Mboto.
Aidha, viongozi wa kiroho nao hawakubaki nyuma kupongeza uwepo wa Tamasha hilo Diamond, Jamhuri- Dodoma na Kirumba-Mwanza. Mchungaji wa kanisa KKKT, mkoani Dodoma, Timothy Holela, anatoa wito wa wengi bila kujali dini kujitokeza kwa wingi
ili kuwatia moyo waandaaji.
Naye Askofu wa Kanisa la Mungu, Donald Mhango pia la mkoni Dodoma, anasema kilichomgusa zaidi katika Tamasha hilo, ni sehemu ya fedha kusaidia wenye shida. Ametoa wito kwa wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili na wananchi kwa ujumla wa Dodoma na vitongoji vyake, kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 25 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Anasema, kitendo cha kuchangia wenye mahitaji maalumu kama wajane, yatima na waathirika wa mabomu ya Gongo la Mbotop, ni chema mbele za wanadamu na Mungu.Anakwenda mbali zaidi na kuishauri Kamati ya maandalizi kuendelea kuandaa matamasha kama hayo kwa maana ya kueneza ujumbe wa neno la Mungu na kusaidia makundi maalumu kwenye jamii.
Comments
Post a Comment