RAIS KIKWETE ASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA SHEIKH YAHYA HUSSEIN…!!!

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisikiliza mawaidha wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia jana jijini. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki.
 Mwili wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein ukiswaliwa nyumani kwake kabla ya kuelekea makaburini.
 Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mh. John Cheyo akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
 Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof. Ibrahim Lipumba akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
 Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akitoa wasifu wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
 Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mtoto wa mwisho wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa leo katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akiwasili nyumbani kwa Marehemu Sheikh Yahya Hussein.
Wakinamama wakionekana na huzuni kubwa ya kuondoka kwa kipenzi cha wengi Sheikh Yahya Hussein. 
 Mamia ya waombelezaji wakisiliza mawaidha nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya Hussein.
 Kinamama wakilia kwa uchungu msibani.
 Msafara wa kuelekea makaburini ukiongozwa na mapikipiki.
 Umati wa waombelezaji ukielekea makaburini
 Mwili Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein ukisubiri kushushwa kaburini tayari kwa maziko.
 Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kumzika Mnajimu Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati.
 Mziwanda wa Marehemu Sheikh Yahya Hussein akitia udongo kwenye kaburi la baba yake wakati wa mazishi.
 Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Mh. Nape Mnauye akishiriki katika mazishi ya Sheikh Yahya Hussein.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia uratibu na uhusiano Mh. Steven Wassira akishiriki katika mazishi ya Mnajimu Mashuhuri wa Afrika ya Mashariki na Kati Sheikh Yahya Hussein.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Suleiman Kova akishiriki Mazishi ya Sheikh Yahya Hussein aliyezikwa leo Alasiri jijini Dar.

Picha kwa hisani ya MOBLOG

Comments