URBAN PULSE inawaleta Ziara ya Mwenyekiti wa Tanzania Assocciation UK Dr Lusingu akifanya ziara ya kutembelea Watanzania wafanyao shughuli mbalimbali hapa England. Dr Lusingu alifuatana na Mjumbe wa NEC Bi Asha Baraka ili naye ajionee na kujifunza wayafanyayo Watanzania UK. Kampuni hii ya Computer 4 Africa inamilikiwa na mjasirimali wa Kitanzaniana aitwae Bw Aseri Katanga. Kampuni hii inajishughulisha na ukusanyaji wa kompyuta zilizotumika, kisha wana zi karabati na kuziweka kwenye hali ya kuwa mpya, halafu wanazisambaza Afrika nzima. Kompyuta hizi hupelekwa kwenye mashule, taasisi mbalmbali na idara ya serikali. Kwa upande wa Tanzania zaidi ya shule 100 zimesha faidika na mpango huu.
mwenyekiti akipata maelekezo kutoka kwa enginer wa kampuni ya computer 4 Africa.
computer zilizofanyiwa urekebishwaji na matengenezo tayari kwa kuingia Africa
Mkurugenzi wa Aset akiangalia moja ya kifaa kinachotumika wakati wa matengenezo
mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu na Asha Baraka wakiangalia baadhi ya Computers
Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akikagua baadhi ya computer zinazosafirishwa na kampuni ya Computer 4 africa
Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka akiteta jambo fulani pamoja na wafanyakazi wa computer 4 Africa na Mwenyekiti wa Tanz UK
picha ya pamoja wa wakurengenzi na wafanyakazi wa Computer 4 Africa wakiwa na mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu na Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka
baada ya kumaliza ziara kutoka kushoto Ndg Katanga, Dr John Lusingu, Frank Eyembe na Asha Baraka
Hii ni Video fupi ya Ziara iliyofanywa na Tanz UK ikiwakilishwa na mwenyekiti wake Dr John Lusingu alieambatana na Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka. Ziara hii iifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa dhumuni ya kutembelea kampuni ya Computers 4 Africa chini ya uongozi wa mwenyekiti Aseri Katanga ambayo inajishughulisha na ukusanyaji wa computer zilizotumika kutoka katika mashirika na taasisi mbalimbali hapa UK, kisha kuzisafisha, kuzikarabati na kuziongezea uhai mpya unaonendana sambamba na teknolojia mpya na mwishowe kuzisambaza Africa Nzima. Tanzania ni mojawapo ya nchi za kiafrika ambazo zimenufaika zaidi katika mpango huu kabambe ambapo shule zaidi ya mia zimenufaika kwa kupewa msaada huu.
Huu ni mmoja wa mifano mizuri ya kuigwa kwa watanzania wote hususani waishio ughaibuni/ Diaspora ili kusaidia kuleta maendeleo nchini kwetu na hatimaye barani afrika bila ya kutegemea serikali pekee.
Habari na picha zote kwa hisani ya URBAN PULSE CREATIVE
Comments
Post a Comment