- Ni Muyahudi mkazi wa Marekani
- Aliacha masomo Havard baada ya kulamba utajiri
Na Blogger team, Andrew Chale,Tanzania
MTANDAO wa Facebook uligunduliwa na mwanafunzi wa masomo ya sayansi wa Chuo Kikuu cha Harvard, Mark Zuckerberg, akishirikiana na wanafunzi wenzake, Eduardo Saverin, Dustin Moskovitz na Chris Hughes.
Mwanzo wa jina la mtandao ndio ulizaa historia ya Facebook. Mtandao huo awali ulifahamika kama Facemash.
Alitumia maarifa yake ya sayansi ya kompyuta vizuri kwa kuingia katika mtandao wa usalama wa Chuo Kikuu cha Harvard na kunakili picha kutoka kwenye vitambulisho vya wanafunzi wenzake vilivyokuwa vikitumiwa katika mabweni ili kuuboresha mtandao wake wa Facemash.
Mtandao wa Facemash ulianza kufanya kazi Oktoba 28, 2003, na ulifungwa siku chache baadaye na uongozi wa Harvard kuupiga marufuku.
Zuckerberg alifunguliwa mashitaka ya kukiuka masuala ya usalama, kukiuka hakimiliki na kukiuka uhuru wa mtu binafsi, kwa kuiba picha za wanafunzi wenzake alizotumia kuutangaza mtandao wake.
Aidha, alifukuzwa katika Chuo Kikuu cha Harvard kutokana na kitendo hicho. Hata hivyo mashitaka yote baadaye yalitupiliwa mbali.
The Facebook
Februari 4, 2004, Zuckerberg alizindua upya mtandao wake na kuupa jina la ‘TheFacebook’.
Siku sita baadaye, Zuckerberg tena aliingia matatani wakati wanafunzi wenzake wa Harvard; Cameron Winklevoss, Tyler Winklevoss na Divya Narendra, walipomtuhumu kuwaibia mawazo yao ya kudhamiria kuanzisha mtandao wa kijamii wenye jina la HarvardConnection, pia kwa kutumia ubunifu wao kutengeneza mtandao wa TheFacebook.
Winklevoss, Winklevoss na Narendra baadaye walimfungulia mashitaka Zuckerberg. Hata hivyo shauri hilo lilimalizwa nje ya mahakama.
Uanachama wa mtandao huo awali ulizuiliwa kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Harvard. Hata hivyo Zuckerberg aliwaandikisha baadhi ya wanafunzi wenzake ili kusaidia kuukuza mtandao wake: Eduardo Saverin alishughulikia mambo ya biashara, Dustin Moskovitz kama ‘programmer’, Andrew McCollum kama ‘graphic artist’ na Chris Hughes. Kwa pamoja timu hiyo iliupanua mtandao huo hadi katika vyuo vikuu na vyuo vingine vya kawaida.
Facebook
Mwaka 2004, mwekezaji, Sean Parker (mwanzilishi wa Napster) alifanywa kuwa rais wa kampuni.
Kampuni ilibadilisha jina kutoka TheFacebook kuwa Facebook, baada ya kununua umiliki wa jina facebook.com mwaka 2005 kwa dola 200,000.
Baadaye Zuckerberg ‘aliuaga umaskini’, baada ya faida ya kampuni yake ya Facebook kumfanya bilionea (mdogo kwa umri) kuliko wote duniani.
Kutokana na jarida la New York Times, Mtendaji Mkuu wa Facebook, Mark Zuckerberg, alichangia dola milioni 100 kwa Newark, ‘New Jersey public school system’, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa na ukata mkubwa.
Maisha ya Zuckerberg
Mark Elliot Zuckerberg alizaliwa Mei 14, 1984, eneo la White Plains, New York, kwa mama Karen, daktari wa magonjwa ya akili na baba Edward Zuckerberg, daktari wa meno.
Yeye na dada zake watatu; Randi, Donna, na Arielle, walikulia Dobbs Ferry, New York.
Akiwa Phillips Exeter Academy, Zuckerberg alishinda tuzo mbalimbali katika masomo ya sayansi (hesabu, astronomy na fizikia).
Akiwa chuoni, Zuckerberg alidai kuwa hajui kuandika wala kusoma Kiingereza, hivyo lugha zake zilikuwa: Kifaransa, Kiibrania, Kilatini na Kigiriki cha zamani.
Anafahamika zaidi kwa kuanzisha mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo yeye ni afisa mtendaji mkuu na rais.
Utaalamu wa kompyuta
Zuckerberg alianza kutumia kompyuta na kuandika software alipokuwa mdogo akisoma shule ya kati.
Baba yake alimfundisha ‘Atari BASIC Programming’ miaka ya 1990, kisha alimkodisha ‘software developer’, David Newman, kumfundisha nyumbani kama mwalimu binafsi.
Newman alimwita mwanafunzi wake ‘mwenye akili nyingi’, kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtangulia.
Zuckerberg pia alichukua mafunzo ya somo hilo katika Chuo cha Mercy, jirani na nyumbani kwao, alipokuwa bado akisoma ‘high school’.
Alifurahia kujifunza programu za kompyuta, hasa vifaa vya mawasiliano na michezo.
Katika programu mojawapo, kwa kuwa baba yake aliyekuwa daktari wa meno na alikuwa akifanyia kazi zake nyumbani, alijenga programu ya ‘software’ aliyoiita ‘ZuckNet,’ ambayo iliruhusu kompyuta zote kati ya nyumba yao na ofisi ya baba yake kuwasiliana kila moja.
Akiwa Harvard
Wakati akianza masomo Harvard, tayari alikuwa ameshajipatia umaarufu mkubwa kama ‘programmer mwenye kipaji’. Alisoma saikolojia na sayansi ya kompyuta.
Katika mwaka wa kwanza wa masomo, aliandika programu aliyoiita CourseMatch, iliyoruhusu watumiaji kufanya uchaguzi wa madarasa ya kusomea na kuanzisha vikundi vya kujisomea pamoja.
Baada ya muda mfupi, alianzisha programu nyingine ambayo awali aliita Facemash, ambayo iliwawezesha wanafunzi kumchagua mtu mwenye sura nzuri kutokana na picha mbalimbali.
Kutokana na mwanafunzi mwenzake aliyekuwa akiishi na Zuckerberg wakati huo, Arie Hasit, anasema keamba alitengeneza programu hiyo kimasihara.
Anasema walikuwa na vitabu vilivyoitwa Face Books, vilivyohusisha majina napicha ya kila mmoja aliyeishi katika mabweni ya wanafunzi.
“Awali, alijenga mtandao huo na kuweka picha mbili tu, au picha mbili za wanaume na picha mbili za wanawake. Waliotembelea mtandao huo walikuwa na hiari ya kuchagua ni nani alikuwa mzuri kuliko wengine.
Mtandao huu ulikuwa wazi kwa siku za mwishoni mwa wiki, lakini Jumatatu asubuhi chuo kilikuwa kinaufunga kwa sababu umaarufu wake ulikuwa unafanya mtandao wa chuo kuelemewa kutokana na wanafunzi wengi kuupenda.
Aidha, wanafunzi wengi walilalamika kwamba picha zao zilikuwa zikitumiwa bila idhini.
Zuckerberg aliomba radhi hadharani, huku wanfunzi wenzake wakizidi kuuulaani mtandao wake kutowatendea haki.
Wakati wa mtandao huo wa ‘utani’ wa Zuckerberg, hata hivyo wanafunzi tayari walikuwa wamekiomba chuo kutengeneza mtandao kama huo ambao ungekuwa na picha na maelezo, ikiwa ni sehemu ya mtandao wa kompyuta za chuo chao.
Kutokana na mwanafunazi mwenzake, Hasit, anasema, “Mark aliyasikia maombi haya nakuamua kwamba kwamba kamachuo kingefanya hivyo, yeye angetengeneza mtandao mzuri kuliko huo ambao chuo kilitarajia kutengeneza.”
Hivyo mtandao wa, Zuckerberg wa Facebook chuoni hapo ulianza kama “Kitu cha Harvard” hadi Zuckerberg alipoamua kuusambaza katika shule nyingine, akimworodhesha aliyekuwa akiishi naye chumba kimoja, Dustin Moskovitz kama msaidizi wake.
Kwanza alianzia Stanford, Dartmouth, Columbia, New York University, Cornell, Brown, na Yale, kisha katika shule nyingine ambazo zilikuwa na uhusiano wa kijamii na Harvard.
Makala hii imetayarishwa kwa msaada wa mtandao.
Kwa maoni na ushauri: Simu 0715715271 au kunyara@gmail.com
Mwisho
Utata wa kisheria
Tuhuma dhidi ya Facebook
Shitaka la ConnectU
Wanafunzi wa Harvard; Cameron Winklevoss, Tyler Winklevoss, na Divya Narendra walimtuhumu Zuckerberg kwa makusudi kuwafanya waamini kuwa angewasaidia kujenga mtandao wa kijamii ulioitwa HarvardConnection.com (badaye uliitwa ConnectU).
Walimfungulia mashitaka mwaka, 2004 lakini kesi ilitupiliwa mbali mwaka Machi 28, 2007.
Ilifunguliwa tena katika federal court mjini Boston. Facebook counter sued in regards to Social Butterfly, a project put out by The Winklevoss Chang Group, an alleged partnership between ConnectU and i2hub.
Juni 25, 2008, kesi iliamuliwa na Facebook alikubali kuhamisha zaidi ya milioni 1.2 common shares na kulipa dola milioni 20 kwa kila moja.
Shitaka la Saverin
Shitaka lililofunguliwa na Eduardo Saverin dhidi ya Facebook na Zuckerberg ilimalizwa nje ya mahakama.
Ingawa makubaliano yaliyofikiwa hayakuwekwa wazi, kampuni ilimthibitisha Saverin nafasi yake kama mmoja wa aanzilishi wa Facebook. Saverin alisaini mkataba ambao haukuwekwa wazi baada ya kufikia maafikiano.
Zuckerberg ni nani?
Mark Elliot Zuckerberg alizaliwa
Mei 14, 1984, White Plains, New York, Marekani.
Mkazi wa Palo Alto, California
Asili yake: Muyahudi
Elimu: Alma mater Harvard College (aliacha masomo mwaka 2004)
Kazi: Mtendaji Mkuu/Rais wa Facebook
(anamiliki asilimia 24 mwaka 2010)
Utajiri fedha taslimu dola 13.5 bilioni (2011)
Ndugu: Randi, Donna and Arielle (sisters)
Tuzo: Time Person of the Year 2010
Website
unajua mambo mengine yanakuwa hayana umuhimu kivile kuweka kwenye blog coz kama kuna ambao hawajui tho sisi TUNAJUA ...wikipedia ipo na vile vile Movie yake ipo pamoja na kitabu....inakuwa pointless kuweka tena historia yake kwenye blog..Zuckerberg anakupotezea tu space mama...hiyo ni kazi ya Wikiepedia
ReplyDeletekwani wewe mbona ni mpumbavu hii mbona imeandikwa kwa kiswahili kuna watu hawajui english tatizo lako nijuu ya nini mama ur blog is decent nawewe fungua blog yako uweke ambavyo haijawahi kuandikwa
ReplyDelete