BREAKING NEWS; SIMBA FC KUINGIA FAINALI KAGAME CASTLE CUP...!!!

  • Timu ya soka Simba Sport Club imefanikiwa kuingia fainal za michuano ya KAGAME CASTLE CUP baada ya kuifunga timu Eli Merelkh ya Sudan bao 5-4 za penalty.



Na Blogger Team, Andrew Chale, Tanzania
Mpira huo ambaao ulikuwa mkali kwa timu zote kucheza kwa kasi, timu hizo ziliweza kufungana 1-1 kipindi cha kwanza  ambapo magoli hayo yalidumu mpaka hatua ya mwisho na kipindi cha nyongeza cha dk 30 kumalizika  hivyo hivyo. 

Mchezo huo ulienda hatua  ya matuta ambapo timu zote zilipiga penati na kupata nne kila timu huku zikikosa moja kwa kila timu,, hatua ya pili ya mikwaju hiyo Simba iliweza kupachika bao kwa mpigaji wake penati, Ulimboka Mwakingwe huku wasudan hao wakikosa kupachika bao baada ya kipa namba one Tanzania 'TANZANIA ONE' Juma Kaseja kudaka penati iliyopelekea ushindi Simba FC....

Kwa matokeo hayo, Simba inasubiri kucheza fainali baina ya timu ya Yanga ama St.George ya Ethiopia mchezo ambao utachezwa hapo kesho uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
This is it! (Picha kwa hisani ya Michuzi)

Comments