Kiwanja cha maonyesho ya kilimo cha John Mwakangale Mbeya
Zimebaki siku chache tu kuanza kwa maonyesho ya kilimo yaani sikukuu ya wakulima nane nane huku kukiwa hakuna dalili zozote za kuanza kwa maandalizi hayo maonyesho hayo yataanza tarehe 1 August mpaka August 8 2011
Baadhi ya mabanda yakiwa yamezungukwa na nyasi kuashiria kuwa mambo bado
Baadhi ya Mabanda yaliyo kuwisha kamilika
Banda La kilimo la Wilayani Chunya
Na Mwandishi wetu
Wakulima 50 kutoka halmashauri za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki katikakuonesha shughuli za kilimo katika meonesho ya wakulima NANENANE ambayo yanatarajia kuanza agasti mosi mwaka huu kwenye uwanja wa JOHN MWAKANGALE.
Meneja wa uwanja wa maonesho hayo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bwana KASILATI MWAKIBETE amesema kuwa halmashauri zote zimethibitisha ushiriki wao na kwamba hatua inayoendelea hadi sasa ni ya kushindanisha wakulima katika shughuli za kilimo.
Kauli mbinu ya maonesho ya kilimo nanenane mwaka huu KILIMO KWANZA TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE.
Comments
Post a Comment