BREAKING NEWS!!! STEVE JOBS CEO WA APPLE AJIUZULU...!!!

Bodi ya wakurugenzi wa Apple imetangaza dakika kadhaa zilizopita kwamba mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Apple amejiuzulu kutoka kwenye kiti hicho na nafasi yake kuchukuliwa na Tim Cook.
Chini ya uongozi wake Apple  imefanikiwa sana kwa ubunifu wao mkubwa waliouonyesha kwenye product zao kama iPhone, iPod, iPad na iMac hongera kwa mzee huyu mwenye upeo mkubwa. Moja ya mafanikio makubwa ikiwa ni kuipita Microsoft na kuongoza kama kampuni kubwa na kabambe ya teknolojia kupita zote duniani
Jobs ambaye ni mmoja wa waanzilisi wa Apple amekuwa akisumbuliwa na Cancer toka mwaka 2004. Kutokana na hali yake ya kiafya,  amekuwa akichukua likizo za mara kwa mara kutoka kazini.
Japokuwa sasa Jobs amepewa nafasi ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Apple, sioni ubunifu wa kampuni hii ukiendelea kwa muda mrefu. Kutokana na imani waliyonayo wawekezaji kwamba Jobs ndio uti wa mgongo wa Apple, naamini kuanzia kesho asubuhi thamani ya Apple itashuka sana. Naamini nafasi ya uenyekiti aliyopewa Jobs ni mbinu tu ya kuwahakikishia wawekezaji kwamba mtaalam bado yupo. Lakini hali yake ya kiafya sio nzuri kabisa na amekuwa akiishiwa nguvu siku hadi siku.
Habari hii si ya kuridhisha kwa wawekezaji na wapenzi wa Apple ila kwa makampuni washindani wa teknolojia watakuwa wameipokea habari hii sio kwa furaha bali kwa tabasamu la upande mmoja.
Apple inategemea kutoa toleo jipya la iPhone 5 hivi karibuni hivyo kwa habari zaidi kwa kile kitakachojiri hapo baadaye tembelea blog yako ya tecknolojia:

Comments