SAFARI YA KUMSAKA MISS VODACOM TANZANIA 2011 YAPAMBA MOTO...!!!

Family Day kwa Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011

JANA ilikuwa ni siku ya warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania kutembelewa na ndugu na jamaa zao kutoka sehemu mbalimbali ambapo waliwatembelea katika hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi pia walipata nafasi ya kucheza muziki na kundi la wanne star.


ZIARA YA VODACOM MISS TANZANIA NGORONGORO

Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakicheza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Wasichana ya Enyorrate E.Ngai inayoendeshwa na Masista iliyopo Monduli Juu mkoani Arusha. 
 Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
 Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika katika lango kuu la kuingilia hifadhi ya Bonde la Ngorongoro. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha katika kibao cha Shule ya Wasichana Maasae iliyopo Wilayani Monduli baada ya kutembelea shule hiyo juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo.
 Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiangalia wanyama wakati warembo hao 30 walipotembelea Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro kujionea maajabu mbalimbalimbali yaliyomo katika hifadhi hiyo. 
Warembo wanaoshiriki la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakikabidhi msaada wa chakula kwa mlemavu, Nanyakwa Olumindi, anae Hudumiwa katika Kituo cha Huduma ya Walemavu Monduli juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo na kufanya shughuli za kijamii. 
Warembo wanaoshiriki la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakimpa ndizi mlemavu, Melkiori Mamasita, anae Hudumiwa katika Kituo cha Huduma ya Walemavu Monduli juzi. Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo katika mikoa hiyo na kufanya shughuli za kijamii.
Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Erikisongo iliyopo Wilayani Monduli.


Vodacom Miss Tanzania watembelea mitambo ya Vodacom Kanda ya Kaskazini



Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzanzia 2011, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Nguvu Kamando akiwapa maelezo mbalimbalimbali kuhusiana na mitambo ya kurushia mawasiliano ya simu ya kampuni hiyo iliyopo mjini Arusha wakati warembo hao walipotembelea kituo hicho. Warembo hao wapo katika ziara ya kimafunzo na kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani Kanda ya Kaskazini.

Comments